Ilikuwa ni siku ya pambano kati ya Sikinde na Msondo katika ukumbi wa Diamond Jubilee, nikiwa na camera yangu nikabahatika kurekodi kitu hiki kitamu sana...tufurahi wote. Usisahau kusubscribe na ku like ili niwe na nguvu za kuendeleza Tanzania Music Channel hii.
MUSIC IN TANZANIA
Histories and stories on Tanzanian urban music
Thursday, March 9, 2023
MIAKA KADHAA ILIYOPITA MSONDO NGOMA WALIKUWA JUKWAANI PALE LEADERS CLUB, ILIKUWA SIKU YA WACHAGA
KATIKA MAKTABA YANGU NIMEKUTA VIDEO HII YA MSONDO NGOMA BABA YA MUZIKI TANZANIA. SIKU HII WALIKUWA JUKWAANI LEADERS CLUB KUSHEREHEKEA 'CHAGA DAY'. HEBU TUFURAHI PAMOJA. LAKINI USIKOSE KUSUBSCRIBE CHANNEL HII ITAKAYOKULETEA MAMBO MENGI YA MUZIKI WA ZAMANI, KAMA UNANENO ONGEA AU ULIZA
Wednesday, March 8, 2023
HATIMAE MSHINDI WA KWANZA NA WA PILI WA TOP TEN SHOW 1988
HAWA hapa ndio waliokuwa washindi wa Top Ten Show 1988 Salna 5 Brothers toka Tanga na MK Group. Bahati mbaya bendi zote zilizofikia kumi bora mwaka ule (1988), International Safari Sound (Ndekule), Mwenge Jazz band, Varda Arts, Super Matimila, Tancut Almasi Orchestra, Vijana Jazz Band, Maquis Original, Sambuluma Band, Salna Brothers na MK Sound. Ni Mwenge Jazz band na Varda Arts tu ambao wanafanya maonyesho mpaka leo. Vijana Jazz Band haieleweki kama bado iko au ndio nayo imekufa rasmi.
Hebu sikiliza kilichojiri.
KAMERA YANGU ILIREKODI DDC MLIMANI PARK WAKIPOROMOSHA KIBAO HIBA
SIKU HII ILIKUWA UMETAYARISHWA MPAMBANO KATI YA MSONDO NA SIKINDE KATIKA UKUMBI WA DIAMOND JUBILEE.....KAMERA YANGU IKAREKODI WANA DDC MLIMANI PARK...HEBU FAID 'LIVE' HII UTADHANI IMEREKODIWA STUDIO. WALALE PEMA WOTE WALIOTANGULIWA MBELE YA HAKI
Tuesday, March 7, 2023
LEO TUSIKIE WALIOKUWA WASHINDI WA NNE NA WATATU WA MASHINDANO YA BENDI YA TOP TEN SHOW 1988
LEO TUNASHUKA KUSIKILIZA NI AKINA NANI WALISHIKA NAFASI YA NNE NA TATU TOP TEN SHOW MWAKA 1988....
Saturday, March 4, 2023
MSHINDI WA SITA NA WATANO MASHINDANO YA BENDI MWAKA 1988
Katika mashindano ya kwanza kila bendi ilipewa uhuuru wa kuchagua nyimbo moja ambayo ishiriki katika mashindano hayo. Katika mashindano ya pili bendi zilipewa nafasi tatu, ya kwanza ni wimbo wowote ambao bendi ingechagua nafasi ya pili ilikuwa ni wimbo wenye'tuni' asili na wimbo wa tatu ulipea jina Afrika Nakulilia.
Mashindano ambayo mnayasikia hapa ni ya shindano la kwanza la 1988. Nategemea wote tunaenda sawa sasa
Friday, March 3, 2023
MATOKEO YA TOP TEN SHOW MSHINDI WA 8 NA WA 7...Varda Arts na Super Matimila
Katika mtiririko wa washindi wa Top Ten Show, Mwenyekiti wa jopo la majaji Dr Alex Khalid aliwatangaza Varda Arts na wimbo wao Tazama Tanzania kuwa ni washindi wa 8, na Super Matimila na wimbo wao Muziki asili yake wapi kuwa washindi wa 7. Sikiliza hapa live kilichojiri siku hiyo.......kumbukumbu kutoka maktaba ya John Kitime
Thursday, March 2, 2023
MATOKEO YA WASHINDI WA TOP TEN SHOW...SIKILIZA MSHINDI WA 10 NA WA 9
MOJA ya changamoto ya TOP TEN SHOW ilikuwa ni urefu wa mashindano yenyewe yalianza mwaka 1988 na kuisha mwishoni mwa mwaka 1989. Sikiliza hapa jinsi walivyotajwa washindi na nyimbo walizopiga live baada ya kutajwa.
10. Orchestra Safari Sound Ndekule - Elimu ni msingi wa maisha
9. Mwenge Jazz band - UKIMWI
Toa maoni ............
Wednesday, March 1, 2023
HOTUBA YA DR ALEX KHALID KWENYE FAINALI YA TOP TEN SHOW 1988, UTADHANI ANAONGELEA HALI YA LEO (Part 1)
MWISHONI mwa mwaka 1989 na mwanzoni mwa 1990 lilifanyika shindano kubwa la kupata nyimbo bora lililojulikana kama Top Ten Show. Bendi nchi nzima zilishiriki, RTD ilipita mikoa mbalimbali na kurekodi maonyesho 'live' ya bendi ambazo zilikuwa ndani ya mashindano hayo. Hatimae siku ya kilele ilifika, sasa hebu sikiliza hapa uchambuzi wa mwenyekiti wa jopo la majaji wa shindano lile Marehemu Balozi Dr Alex Khalid akichambua yaliyojiri, utadhani anaongelea muziki wa dansi leo, miaka 42 baadae.
Je ina maana bendi bado ziko palepale zilipokuwa 1988?
Toa maoni yako
Tuesday, January 10, 2023
MAQUIS ORIGINAL WAJIKUSANYA TAYARI KWA MAONYESHO MAKUBWA MAWILI YA PAMOJA
BENDI kongwe iliyokuwa maarufu sana, Maquis Original itauanza mwaka huu kwa kufanya maonyesho mawili makubwa ya kumbukizi ya enzi zake. Maquis Original awali ilikuwa ikiitwa Maquis du Zaire wakati ikiingia nchini Tanzania kwa mara ya kwanza, ilikuwa ikitokea mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati huo nchi hiyo ikiitwa Zaire. Baada ya kuwasili Tanzania, haikupita muda mrefu bendi ikawa moja ya bendi tishio nchini. Nyimbo za bendi hii hata zile ilizo rekodi mwanzoni baada ya kuingia nchini bado ni nyimbo pendwa kwa waliokuweko enzi hizo na hata ambao wamezaliwa miaka mingi baada ya bendi kuwa imepotea katika ulimwengu wa muziki. Uamuzi wa wanamuziki wa bendi hii kujikusanya na kufanya maonyesho yao hakika ni faraja kubwa kwa wapenzi wa bendi hii. Bendi itafanya maonyesho mawili. Onyesho la kwanza litakuwa tarehe 21 Januari 2023 katika ukumbi wa Break Point Makumbusho na tarehe 27 January katika ukumbi wa Royal Village Dodoma
MAMBO MATAMU YAJA
Hebu tukumbuke enzi hizo kwa kuangalia tangazo la dansi la Orchestra Maquis miaka hiyo ambalo nina uhakika litaleta kumbukumbu kwa wapenzi wa Maquis wa enzi hizo za Mtindo wa Telemka Chekecha Scania LBT III, wakati huo gari za Scania ndizo zilikuwa maarufu nchini na Scania LBT III ilikuwa gari yenye saiz kubwa kuliko zote, na ndio yenye kusifika zaidi. Maquis walikuwa na ufadhili wa kampuni hiyo ya magari, ukumbi wa nyumbani wa bendi hii wakati huo ulikuwa ukumbi wa White House uliokuwa Ubungo. Karibuni tena wapenzi wa White House mchangie, mambo yalikuwa mazito chini ya uongozi wa Chinyama Chiyaza ambae alikuwa mpiga Saxophone katika bendi. Wakati huu Maquis ilikuwa na maendeleo makubwa sana ya kuwa na mashamba, magari, matrekta na hata kuwa na Kota zake pale Sinza Palestina. Hebu angalia majina ya wanamuziki waliokuwa kwenye bendi hiyo, wote walikuwa miamba ya muziki.
Thursday, December 22, 2022
WASIFU WA MAREHEMU RAMADHANI KINGUTI - KINGUTI SYSTEM
Marehemu Ramadhan Maulid Kinguti maarufu kama Kinguti System
ni mzaliwa Ujiji, Kigoma. Alikuwa mtu aliyependa sana utani na ucheshi.
Bendi yake ya kwanza aliyojiunga mwaka 1977, ilikuwa Super
Kibisa iliyokuwa na makao yake makuu Kigoma. Super Kibisa ni bendi iliyoanzishwa mwaka 1968 pale
Kigoma. Mwaka 1977 kiongozi wa bendi alikuwa Mlolwa Mussa Mahango ambaye
alikuwa ni binamu yake Ramadhani Kinguti, na
hivyo ikawa rahisi kwake kujiunga
na bendi ile. Super Kibisa ilikuwa mali ya watu watatu, Gollo Saidi, Haruna
Mahepe, na Maulidi. Katika bendi ya Super Kibisa, kipaji cha utunzi cha Kinguti
kilianza kujitokeza mapema na aliweza
kutunga nyimbo kadhaa kama vile Kazi ni uhai, Mapenzi tabu,na Zaina.
Miaka miwili baadae, 1979, Kinguti alichukuliwa na Ahmed
Sululu ambae alikua Katibu wa bendi ya
Dodoma International na kuhamia Dodoma. Dodoma International ilimchukua
Kinguti ili kujaza nafasi ya Shaaban Dede ambaye alikuwa kahama bendi hiyo na
kuhamia JUWATA.
Alipofika Dodoma international , Kinguti alikutana kwa mara ya kwanza na mpiga gitaa
mahiri marehemu Kassim Rashid. Kinguti aliiacha Dodoma International Orchestra
na kujiunga na Orchestra Makassy ambapo
wakati huo walikuweko wanamuziki akina Marehemu Masiya Radi, mwimbaji Mkongo ambaye alifariki kwa kukanyagwa na
daladala maeneo ya Kinondoni Mbuyuni. Baadhi ya wanamuziki wengine ambao
Kinguti alikuwa nao alipokuwa Orchestra Makassy walikuwa marehemu Remmy Ongala, marehemu Andy Swebe, Keppy
Kiombile, John Kitime, marehemu Issa Nundu, marehemu Kyanga Songa, Choyo
Godjero na wengineo, pia alikuweko marehemu Aimala Mbutu kwenye solo, na Kassim
Mganga (babake wa mwanamuziki wa Bongo flava Kassim Mganga-Milionea wa Mahaba)
kwenye rhythm, na wengine wengi. Kwa
kipindi fulani muda huu Kinguti akiwa na wenzake chini ya Mzee Makassy
wakafanya ziara ndefu nchini Kenya, kati ya waliokuwepo katika safari hiyo ni
Nico Makoli, Keppy Kiombile, Andy Swebe,
Mzee Aimala Mbutu, Mzee Liston na wengine wengi akiwemo Mzee makassy mwenyewe.
1986 alijiunga Afrisongoma chini ya Lovy Longomba, hapa
alitunga nyimbo kadhaa kama Pesa ni maua, Amana mpenzi, Estah Usituchonganishe,
waimbaji wakati huo walikuwa Kinguti, marehemu Lovy Longomba na Anania Ngoliga, kwenye solo alikuweko
marehemu Kassim Mponda, na rhythm Maneno Uvuruge. Kwa muda mfupi alikuwa DDC
Mlimani Park, na hapa akatunga kile kibao maarufu Visa vya mwenye nyumba,
ambapo aliimba na Hassan Bitchuka, Francis Lubua, Hussein Jumbe na Benno Villa.
Mwaka 1989 alikuwa moja ya wanamuziki waanzilishi wa Bicco Stars Band akiwa na
Mafumu Bilali, Asia Darwesh, Andy Swebe, Mzee Aimala Mbutu, walitikisa na vibao
kama Muuza chips, Leyla, Magreth maggie, Kitambaa cha kichwa, Nyumba ya
kifahari, na nyingine nyingi tu. 1999 alijiunga na kilimanjaro Connection,
alikaa bendi hii iliyokuwa chini ya Kanku Kelly kwa miaka miwili kisha
kuanzisha bendi akiwa na Hassan Shaw, bendi iliyoitwa The Jambo Survivors
ambayo wengi hapa Tanzania wataikumbuka kwa kibao cha Maproso. Bendi ya Jambo
Survivors ikiwa bado na Ramadhan Kinguti na Hassan Shaw, kwa miaka kadhaa
ikahamia Thailand. Baada ya kurudi Thailand afya ya Kinguti ilikuwa na migogoro
mingi hivyo hakurudi tena kwenye muziki na muda mwingi alikuwa Dar es Salaam
kisha Kigoma.
Ramadhani Kinguti amefariki tarehe 21 Disemba 2022 katika
hospitali ya Maweni Kigoma, na mazishi ni tarehe 22 Disemba 2022 hapohapo
Kigoma
Mungu amlaze Pema.
Sunday, December 18, 2022
TWO DAYS AFTER REMMY ONGALA DIED, HIS DRUMMER FOLLOWED HIM
The late Abou Semhando. |
It was
around three o'clock at night, on Saturday 18 December 2010, when I got
a call from veteran musician Luiza Nyoni, she was crying and told me that there
had been an accident and Abou Semahando who was on a motorcycle had been hit by a
car and had died, the accident had happened in Mbezi Tanki Bovu. I
woke up and went to the accident site and alas the information was true.
I found Abou's motorcycle had already been loaded in a police car and the car that had hit him was
in the ditch.
The car |
Abou Semhando first on right with a red shirt, in a group photo with fellow musicians during the Dr Remmy's funeral ceremony |
Timetable for funeral arrangements for the late Abou Semhando (Baba Diana), musician and manager of the African Stars Band-Twanga Pepeta
• Saturday
18/12/2010-friends and relatives gathered at the home of the deceased,
Mwananyamala Kisiwani (Ngilangwa) to offer condolences and console the
bereaved.
• Sunday
19/12/2010- 5:00 AM. Dawn prayers at Muhimbili mosque, after the prayer
the mourners would travel to Kibanda, Muheza ready
for the funeral.
•
Immediately after lunch the body would be moved to the Muheza mosque and after
prayer the body would be taken to the cemetery for burial.
• Mourners
would return to Dar es Salaam after the burial.
Some notable things:
1.19/12/2010 was the day his eldest daughter was to be married
2. He had
written to the management of the Band to give him a month's leave because he
wanted not to be on stage for a while. It is the first time he wrote a letter
requesting leave
3. The
ringtone he put on his phone is the song by Njohole Jazz Band - this band's
musicians almost all died together in a bad car accident.
Standing from left to right -.Remmy Ongala, Abuu Semhando,Kasaloo Kyanga, Fan Fan they are all deceased. |
I first met Abou Semhando around 1979, we were both working with Printpak Tanzania Ltd, he was in typesetting department I was a proofreader. At the time he was with Sola TV Band I was with the Oshekas Band, but I would honestly say we were not close in any way. In 1989 I joined the Vijana Jazz band he was the band's second in command and we became quite close after. In his lifetime Abou was a member of several bands including Sola TV, Vijana Jazz, Diamond Sound and Super Matimila.
Abou Semhando : You will follow and back his songs like you always did.
Cosmas Chidumule: No way, you should follow him after all you were his drummer for a longer period.
Two days later it was a joke no more Abou went on to join his comrade
MAY GOD
FORGIVE THEIR SHORTCOMINGS
AMEN